BiasharaChina
Rais Xi Jinping atoa wito wa ushirikiano na Marekani
27 Machi 2024Matangazo
Mkutano huo unafanyika wakati mahusiano kati ya mataifa hayo mawili yakiaanza kuimarika baada ya kudorora kwa miaka kadhaa.
Xi amesisitiza leo kuhusu mahusiano hayo ya kiuchumi yenye manufaa kwa mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa zaidi duniani, licha ya ushuru mkubwa unaotozwa na Marekani kwenye manunuzi ya bidhaa za China.
Xi amenukuliwa na shirika la habari la nchi hiyo Xinhua akisema kuwa mahusiano ya China na Marekani ni moja ya mahusiano muhimu zaidi kati ya mataifa mawili kote duniani na yanayotoa mwelekeo wa siku za baadaye.
Washiriki katika mkutano huo ni pamoja na Stephen A. Schwarzman, mkuu wa kampuni ya uwekezaji ya Blackstone.