Yaa Nana Asantewaa - Malkia wa vita
Yaa Asantewaa aliishi katika miaka ipi? Alizaliwa mwaka 1840 katika mji wa Besease, wakati wa ufalme wa Ashanti. Alifariki dunia akiwa uhamishoni katika visiwa vya Shelisheli tarehe 17 Oktoba mwaka 1921.
Anatambulika kwa: alivyochochea na kuunga mkono kile leo kinachoitwa vita vya kiti cha dhahabu. Kiti hicho cha dhahabu kilikuwa moja ya vitu vya kuogofya katika umiliki wa Asante, na mwakilishi wa Uingereza kwa wakati huo Bw. Fredrick Mitchel Hodgson alitaka kiletwe kwake ili akikalie kwa jina la Malkia wa Uingereza.
Kuteuliwa na wafalme wengi wa Mkoa wa Asante kuwa kiongozi wa vita wa Jeshi la mapigano la Asante - kama mwanamke wa kwanza katika historia ya Asante
Kuwa katika mstari wa mbele kwenye vita kwa nyakati tofauti kutoa ushauri na kusafirisha vifaa kwa wapiganaji wa Asante - akiwa na umri wa miaka 60.
Akitoa maoni juu ya kushindwa kutenda kwa ustadi kwa wanaume wa Asante kuhusiana na ombi la mwakilishi wa Uingereza:
"Siwezi kuamini. Haiwezekani! Lazima niseme jambo hili; Kama nyie wanaume wa Asante hamtasonga mbele, basi tutafanya hivyo. Nitawaita wanawake wenzangu. Tutapigana na wazungu. Tutapiambana hadi mwisho wetu sisi uwe uwanja wa vita. Kama wakuu hawawezi kupigana, mnapaswa kubadilishana nguo zenu za kiunoni na nguo zangu za chini"
Anakubwa kwa: Yaa Asantewa ni mfano muhimu na msukumo kwa wasichana na wanawake wengi nchini Ghana na afrika kwa ujumla kwasababu ya ujasiri aliouonyesha. Wanawake wengi ambao wanafanya kazi ambazo hapo awali zilikuwa zikitawaliwa na wanaume mara nyingi wamepewa jina la Yaa Asantewaa ikiwa ni njia ya kuwatia moyo na kuwaunga mkono.
Mnamo mwaka 2000, makumbusho moja ilijengwa kwa kumbukumbu ya malkia huyo wa vita huko Ejisu. Familia yake ilikuwa na ukarimu wa kutosha kuchangia vitu maalum vya urithi na makala ambazo Yaa Asantewaa alivitumia, ikiwemo nguo, gamba la kobe ambalo inaaminika alikuwa akitumia kulia chakula. Kwa bahati mbaya, makumbusho hayo yaliungua kwa moto Julai 2004. Vitu vingi vilipotea na makumbusho hayo bado yamesalia tupu.
Shule ya kwanza ya serikali mjini Kumasie ilipewa jina la: Shule ya sekondari ya wasichana ya Yaa Asantewaa.
Pinado Abdu-Waba, Ramatu Mahmud Abubakar Jawando na Gwendolin Hilse, wamechangia kuandika makala hii. Ni sehemu ya makala maalum za mfululizo wa "Asili ya Afrika", ushirikiano kati ya shirika la DW na taasisi ya Gerda Henkel.
Tafsiri: Sylvia Mwehozi
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman