1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yamousoukro. Jeshi la serikali na la waasi nchini Ivory Coast wapanga siku ya kuwanyang’anya silaha wapiganaji wao.

15 Mei 2005

Jeshi la serikali na lile la waasi nchini Ivory Coast limetia saini makubaliano jana yanayoweka siku ya Juni 27 kuwa ni siku ya kuanza kuwanyang’anya silaha wapiganaji wao.

Maafisa katika taifa hilo la Afrika magharibi wamesema kuwa baada ya juhudi kadha kushindwa katika muda wa miezi kadha, mkuu wa jeshi la Ivory Coast pamoja na mwenzake wa jeshi la waasi walitia saini makubaliano hayo wakiweka sheria na utaratibu wa kuwanyang’anya silaha wapiganaji.

Jeshi la waasi la New Forces limekuwa likishikilia eneo la kaskazini ya nchi hiyo tangu pale lilipotokea jaribio lililoshindwa la kumtoa madarakani rais Laurent Gbagbo mwezi Septemba mwaka 2002 na kuligawa taifa hilo katika sehemu mbili. Pande hizo mbili zinatenganishwa na majeshi ya Ufaransa na yale ya umoja wa mataifa ya kulinda amani.

Makubaliano hayo mapya iwapo yatafanikiwa, yatapelekea kunyang’anywa silaha wanajeshi 42,500 wa jeshi la waasi na wapiganaji 5,500 wa jeshi linalounga mkono serikali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW