1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yanayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati

22 Oktoba 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amewasili nchini Israel kuendeleza hatua zaidi za kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza. Jeshi la Israel limeishambulia kambi ya wanamaji ya Hezbollah mjini Beirut.

US-Außenminister Antony Blinken trifft in Tel Aviv ein
Picha: Nathan Howard/REUTERS

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anafanya ziara nchini Israel siku chache baada ya vikosi vya Israel kumuua kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar. Ziara ya Blinken, ya kikanda inafanyika wiki mbili kabla ya uchaguzi wa Marekani.

Hii leo Blinken atakutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kesho Jumatano ataelekea Jordan ambako anatarajiwa kwenda kujadili kuhusu misaada ya kibinadamu kwa Ukanda wa Gaza, hayo ni kwa mujibu wa afisa mmoja mkuu aliye kwenye safari hiyo ya Blinken.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: dts-Agentur/picture alliance

Nchi nyingine ambazo Blinken huenda akazijumuisha kwenye ziara yake ya mshariki ya kati ni, Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Soma Zaidi:  Israel yasema imewaua wanachama 15 wa Hezbollah

Hii ni ziara ya 11 ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, katika eneo la Mashariki ya Kati tangu vita vya Gaza vilipozuka mwaka jana na wakati huo huo Israel inapozidisha mashambulizi yake dhidi ya Hezbollah nchini Lebanon.

Jeshi la Israel limesema limevishambulia vituo kadhaa vya kuhifadhia silaha vya Hezbollah pamoja na kamandi za kundi hilo usiku kucha wa kuamkia siku ya Jumanne. Jeshi la Israel limesema pia kambi muhimu ya wanamaji inayotumiwa na Hezbollah imeshambuliwa katika mji wa Beirut.

Na huko nchini Iran msemaji wa wizara ya mambo ya nje Ismael Baghaei, amesema wakati Israel inafikiria kulipiza kisasi shambulio la makombora la Iran la Oktoba mosi dhidi ya Israel, nchi majirani wa Iran hazitaruhusu ardhi zao kutumika kwa mashambulio dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Rais wa Iran Masoud PezeshkianPicha: Iranian Presidency/Zuma/picture alliance

Baghaei amesema: "Tunafuraha kwamba sisi na nchi zote za eneo hili tumefikia kiwango hiki kikubwa cha ukomavu na tunakubaliana na mawazo kwamba kulinda amani katika eneo hili ni jukumu letu la pamoja."

Soma Zaidi:  Iran yaahidi kuishambulia tena Israel endapo itashambuliwa

Iran katika siku za hivi karibuni imeongeza juhudi za kidiplomasia, kushinikiza kusitishwa kwa mapigano huko Lebanon na Gaza na pia kutafuta njia za kuzuia mizozo.

Vyanzo: AFP/RTRE

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW