1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yanga yaanza mchakato wa kusaka kocha mpya

20 Oktoba 2025

Klabu ya Yanga nchini Tanzania iko kwenye hatua ya mpito baada ya kuachana na kocha mkuu Romain Folz kwa makubaliano ya pande zote kufuatia matokeo yasiyoridhisha ikiwemo kipigo dhidi ya Silver Strikers ya Malawi.

Kandanda | CAF | Hersi Said na Patrice Motsepe
Mwenyekiti wa chama cha Klabu za Afrika Hersi Said na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe mjini Cairo, MisriPicha: CAF Communications

Klabu ya Yanga nchini Tanzania imeanza rasmi mchakato wa kumsaka kocha mkuu mpya baada ya kuvunja mkataba na Romain Folz, chini ya uongozi wa Rais Mhandisi Hersi Said.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka klabu ya Yanga SC, mkataba wa Romain Folz umevunjwa kwa makubaliano ya pande zote mbili kufuatia matokeo yasiyoridhisha, ikiwemo kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Silver Strikers ya Malawi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kipigo hicho kilikuwa cha kwanza kwa Yanga msimu huu na kilichochea uamuzi wa uongozi chini ya Rais Mhandisi Hersi Said kuanza mchakato wa mabadiliko ya benchi la ufundi.

Aliyekuwa kocha msaidizi, Patrick Mabedi, amekabidhibiwa jukumu la kuiongoza timu kwa muda akisubiri uteuzi rasmi wa kocha wa kudumu.

Hakuna jina lililotangazwa rasmi hadi sasa, lakini vyanzo vya habari vinaeleza kuwa majina kadhaa yanachunguzwa kwa kina.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW