1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yangon: Homa ya ndege yagunduliwa tena Myanmar

2 Agosti 2007

Myanmar imetangaza kutokea kwa mara nyingine tena maradhi ya homa ya ndege.

Wakuu wa serikali hiyo wametoa tangazo hilo baada ya kugundua kuku aliyeambukizwa katika shamba lililoko kaskazini mwa mji mkuu, Yangon.

Uchunguzi wa maabara wa Jumanne iliyopita ulithibitisha kuweko kiasi bata watatu na kuku wanne walioambukizwa virusi vya homa hiyo kwenye shamba la kibinafsi.

Kuku karibu elfu nne wamechinjwa ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

Siku ya Jumapili iliyopita mashamba mawili yaligunduliwa yalikuwa yameambukizwa virusi hivyo katika jimbo la Mon, kilomita mia moja na themanini kusini mashariki ya Yongon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW