1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON:Jenerali Than Shwe akubali kukutana na Aung San Suu Kyi

4 Oktoba 2007

Kiongozi wa kijeshi wa Myanmar Jenerali than Shwe anakubali kukutana na kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi ila kwa masharti.Alimueleza hayo mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa ili kuonyesha kuwa serikali ina nia ya kujadiliana na uoinzani baada ya kukabiliwa na upinzani mkubwa katika kipindi cha miaka 20.

Jenerali Than Shwe alimueleza Bwana Ibrahim Gambari kuwa atakutana na Bi Aung San Suu Kyi endapo atafutilia mbali wito wake wa kupambana na serikali na kuiwekea vikwazo.Masharti hayo ya Jenerali Than Shwe si mapya kwani utawala wa kijeshi wa Myanmar umekuwa ukimlazimisha Bi Aung San Suu Kyi kubadili kauli yake ya kutaka serikali hiyo kuwekewa vikwazo.

Hata hivyo ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyo wa kijeshi kukubali kukutana na Bi Suu Kyi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW