SiasaYemen
Zaidi ya mataifa 30 yametoa ahadi ya msaada wa kibinadamu
28 Februari 2023Matangazo
Mratibu wa Misaada ya Dharura wa Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths ametoa wito wa kuendelea na muda wa kuwekwa chini silaha akionesha kuwepo kwa nafasi ya kusitishwa kabisa mapigano.
Grifitths amesema kiwango cha fedha kilichotolewa cha dola bilioni 1.2 sio kile kilichotarajiwa cha dola bilioni 4.3 lakini Umoja wa Mataifa umesema huenda dola bilioni 2 zikapatikana mwishoni mwa wiki hii katika mkutano huo wa wahisani wa kuhamasisha utoaji wa msaada kwaajili ya Yemen.