YONGBYON:Kinu cha nyuklia chalemazwa
6 Novemba 2007Matangazo
Wataalamu kutoka Marekani wameanza kulemaza kinu cha nyuklia cha Yongbyon nchini Korea Kaskazini.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Tom Cassey ameitaja hatua hiyo ya kwanza kuwa ni ya muhimu katika kukifunga kinu cha nishati ya Atomiki cha Yongbyon.
Korea Kaskazini imekubali kuacha uchu wake wa kumiliki silaha za nyuklia na badala yake itapokea misaada na uhakika wa kidplomasia chini ya makubaliano ya pande sita yaliyofikiwa pamoja na Marekani, Korea zote mbili, China Urusi na Japan.