1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Yoon Suk Yeol agoma tena kuhojiwa na timu ya wachunguzi

20 Januari 2025

Rais wa Korea Kusini aliyesimamishwa kazi na Bunge, Yoon Suk Yeol amegoma kuhojiwa leo Jumatatu na timu ya wachunguzi ili kubaini ikiwa alitenda uasi kwa jaribio lake la kuiweka nchi chini ya sheria ya kijeshi.

Yoon
Picha hii inamuonyesha Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol akizungumza mjini Seoul, Korea Kusini, Januari 15, 2025 Picha: South Korean President Office via Yonhap/AP Photo/picture alliance

Mamlaka imesema ulinzi ulikuwa umeimarishwa katika kituo anakozuiliwa Yoon mjini Seoul kabla ya kesi na Mahakama ya Kikatiba ikiwa inashikilia mashtaka ya kesi na kuamua iwapo itamwondoa madarakani kabisa.

Mmoja wa mawakili wa Yoon amesema walipanga kuhudhuria kikao cha kesi ya mashtaka siku ya Jumanne lakini timu ya wachunguzi ilimfuata Yoon hii leo kumhoji kwa nguvu lakini bila mafanikio.

Yoon amekuwa rais wa kwanza wa Korea Kusini aliye madarakani kukamatwa kutokana na tangazo lake la muda mfupi la sheria ya kijeshi mwanzoni mwa mwezi desemba mwaka uliopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW