Yulia Navalnaya asema mumewe alilishwa sumu gerezani
17 Septemba 2025
Matangazo
Katika vidio iliyochapishwa leo, Navalnaya amesema maabara katika nchi mbili zilichunguza kwa njia huru sampuli za kibiolojia zilizosafirishwa kutoka urusi na zote mbili zilifikia hitimisho kwamba Alexei aliuawa, haswa kwa kulishwa sumu.
Navalnaya amesema ana ushuhuda wa wafanyikazi wa gereza la Kharp.
Hakufichuwa matokeo halisi ya uchunguzi huo kwa mfano sumu iliyotumika kumuuwa mumewe katika gereza hilo, badala yake alitaka kuchapishwa kwa ripoti hizo za maabara.
Navalnaya pia amewashtumu wanasiasa wa magharibi, na kusema wamemwambia uchapishaji wa matokeo ya maabara ulikuwa ukiahirishwa kwa sababu za kisiasa.