Yuro milioni moja kwa atakaetoa habari mpaka Mladic akakamatwe
12 Oktoba 2007Matangazo
Belgrade
Jamhuri ya Serbia imetenga yuro milioni moja kama bahshishi kwa yeyote atakaetoa maelezo yatakayopelekea kukamatwa mhalifu mkubwa wa vita Ratco Mladic.Baraza la usalama wa taifa limeamua kutoa fedha hizo kama jaza ya kukamatwa jenerali huyo wa Bosnia mwenye asili ya Serbia.Ratco Mladic anasakwa na korti kuu ya kimataifa ya uhalifu wa vita katika yugoslavia ya zamani.Anatuhumiwa kuhusika na mauwaji ya waislam elfu nane wa Srebrenica.Bahashishi nyengine ya yuro laki mbili na nusu imetengwa kwaajili ya yeyote atakaetoa habari zitakazopelekea kukamatwa watuhumiwa wengine wawili wenye asili ya Serbia, Stojan Zupljanin na mkuu wa waserbia wa Kroatia Goran Hadzic.