1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya asilimia 90 Guinea wapiga kura ya 'ndiyo'

23 Septemba 2025

Zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wa Guinea wamepiga kura ya 'ndiyo' katika kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba inayoweza kumruhusu kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo Jenerali Mamadi Doumbouya, kugombea urais.

Guinea | Übergangspräsident Mamadi Doumbouya
Picha: Souleymane Camara/REUTERS

Akizungumza na waandishi habari, Mkuu wa Tume ya Uchaguzi Djenabou Toure amesema kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa Jumatatu usiku, asilimia 90.06 wamepiga kura ya 'ndiyo' na asilimia 9.04 wamepiga kura ya 'hapana'.

Toure amesema kura hiyo ya maoni ilihitaji takribani asilimia 50 ya wapiga kura ili iweze kupitishwa.

Guinea ni miongoni mwa mataifa yanayozidi kuongezeka Afrika Magharibi ikiwemo Mali, Niger na Burkina Faso ambako jeshi limechukua udhibiti.

Baadhi ya wachambuzi wanasema kura hiyo ya maoni ni njia kwa Jenerali Doumbouya kusaka urais na kuhalalisha utawala wake wa kijeshi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW