Kutokana na matumizi ya maji machafu
1 Septemba 2016Mifumo ya kutibu maji ambayo hutiririka kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na makazi ya watu na viwandani si wa kutumainiwa sasa kwani umekuwa hauyatibu maji hayo inavyotakiwa na hivyo kuwaweka wananchi hao katika hatari ambapo taarifa zinaonyesha kuwa mwaka 1999 na 2010 uchafuzi wa maji ulisababisha virusi, bakteria na sumu za muda mrefu kuongezeka katika nusu ya mito katika mabara hayo
Katika ripoti iliyotolewa na shirika la mazingira la umoja wa mataifa UNEP siku ya Jumanne inaelezwa kuwa ongezeko la watu, kuongezeka kwa maeneo ya kuendeshea shughuli za kilimo na kuongezeka kwa mifumo mibovu ya kusafirisha na kutibu maji taka kuelekea katika mito na maziwa ni moja kati ya sababu ambazo zimechangia kuchafuka kwa maji hali ambayo inawaweka watu hao katika hatari ya kupata maambuki ya magonjwa hayo
Kando na kuwa katika hatari ya kuambukizwa magonjwa kilimo cha umwagiliaji nacho kinakumbwa na changamoto kwa kuwa wakulima hutumia maji ya mito na maziwa yakitokea katika maeneo ya migodini na hivyo kukifanya kilimo hicho kuwa si cha kutegemewa tena kutokana na mavuno hafifu
Dietrich Borchart kiongozi wa safu ya wataalamu wa UNEP walioandika ripoti hiyo ameliambia shirika la habari la wakfu wa Thomson Reuters, kuwa upatikanaji wa maji safi na salama duniani bado ni changamoto kubwa na idadi ya watu wanaothiriwa ni kubwa ikilinganishwa na vile ilivyokuwa ikidhaniwa pamoja na kuongeza kuwa bado kuna baadhi ya mito ambayo haijaathiriwa na hivyo zinahitajika juhudi za kuilinda
"Ni gharama sana kusaifisha maji kutoka katika mifumo michafu iliyokithiri zaidi ya kufanya utekelezaji wa mipango bora zaidi ya kuuzuia uchafuzi," amesema Borchardt na kuongeza kuwa vifaa vipo ila changamoto kubwa ipo katika utekelezaji wa mipango hiyo.
Watu zaidi wako hatarini
Kutokana na kuwa na mifumo mibovu ya kutibu maji taka yanayoelekea katika mito na maziwa mabara ya Afrika, Asia na Amerika Kusini yameathiriwa kwa kiasi kikubwa ambapo Amerika Kusini pekee robo tatu ya mito yake yote imeathiriwa, barani Afrika asilima 10 mpaka 25 ya mito na maziwa imeathirika na huko Asia ni asilima 50 hali ambayo inazidi kuhatarisha zaidi maisha ya wananchi wake
Kwa mujibu wa ripoti hiyo watu milion 3.4 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa kama kipindupindu, homa ya matumbo, polio pamoja na kuhara magonjwa ambayo asili yake ni matumizi ya maji ambayo sio salama na inakadiriwa kluwa watu milion 164 kutoka Afrika, 134 kutoka Asia na milion 25 kutoka Latin Amerika walikuwa katika hatari ya kuambukizwa magonjwa hayo
Inaelezwa kuwa kujengwa kwa mifumo ya ndani kwa ndani ya kusafisha maji hakuwezi kusaidia juhudi za kuwanusuri wananchi hawa badala yake kunahitajika mbinu nyingine zaidi ili kuweza kupata maji salama ambayo yametibiwa ipasavyo
Mwandishi: Celina Mwakabwale/Reuters
Mhariri:Iddi Ssessanga