Zaidi ya nusu idadi ya watu Sudan wanahitaji msaada
15 Novemba 2025
Wiki hii, Katibu Mkuu wa Baraza hilo la Wakimbizi la Denmark Charlotte Slente ameliambia shirika la habari la AFP baada ya ziara yake katika eneo la mpakani mwa Chad na Sudan kwamba alishuhudia hali ambayo zaidi ya watu milioni 30 wanahitaji msaada wa kibinadamu, hiyo ikiwa ni nusu ya idadi jumla ya watu wa Sudan na kusisitiza kuwa "mateso aliyoyashuhudia hayafikiriki."
Sudan inashuhudia ukiukwaji unaovunja sheria zote za kimataifa
Ameongeza kusema eneo hilo linashuhudia ukiukwaji unaovunja sheria zote za kimataifa za kibinadamu na kwamba shirika hilo limeona ushahidi wa mauaji ya watu wengi na unyanyasaji wa kingono nchini Sudan.
Pia amesema watu wamewekwa kizuizini, kutekwa nyara, kulazimishwa kukimbia na mateso
Slente ameishtumu jamii ya kimataifa kwa kutochukuwa hatua za kutosha kuhusu Sudan.