1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMalawi

Zaidi ya nusu ya watoto wanakabiliwa na utapiamlo Malawi

Daniel Gakuba
7 Machi 2023

Umoja wa mataifa umetoa tahadhari kwamba tatizo la utapiamlo linawaweka watoto nchini Malawi katika hatari kubwa ya kukumbwa na maradhi ya kipindupindu, ambayo yameena nchini humo.

 Cholera Jemen
Picha: Mohammed Mohammed/dpa/picture alliance

Makadirio ya shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia watoto, UNICEF yameonyesha kuwa watoto wapatao milioni 4.8, sawa na nusu ya watoto wote katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, wanahitaji msaada wa kiutu.

Ripoti ya shirika hilo imesema kua hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Machi, inatarajiwa kuwa watoto zaidi ya 213,000 watakumbwa na utapiamlo mkubwa, 62,000 miongoni mwao wakiweka katika kundi lenye tatizo lililopitiliza.

Afisa Mkazi wa UNICEF nchini Malawi, Rudolf Schwenk, amesema mtoto anayesumbuliwa na utapiamlo yuko hatarini kufa kutokana na kipindupindu, mara 11 zaidi ya mtoto mwenye afya njema.

Umoja wa Mataifa umeomba kiasi cha dola milioni 50 za kukabiliana na mripuko wa kipindupindu nchini Malawi.