1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya waandamanaji 300 washikiliwa na polisi nchini Kenya

20 Julai 2023

Watu wawili wameuwawa jana na wengine zaidi ya 300 wamekamatwa na polisi wakati wa maandamano ya umma nchini Kenya yanayoongozwa na upinzani.

Kenia Nairobi Gewalt bei Protesten gegen Regierung
Picha: THOMAS MUKOYA/REUTERS

Makabiliano kati ya polisi na waandamanaji ndiyo chanzo cha vifo hivyo kufuatia maandamano yaliyoitishwa na viongozi wa upinzani ambao wamedai kuwa maandamano hayo yataendelea.

Shule za kutwa zimefunguliwa tena baada ya serikali kuhakiki hali ya usalama wa wanafunzi. Kwa upande wao, vinara wa upinzani wa Azimio la Umoja bado hawajaonekana hadharani ila wanasisitiza maandamano yanaendelea.

Wito wa kukaa kwenye meza ya mazungumzo bado unatolewa kuwarai kiongozi mkuu wa upinzani, Raila Odinga na Rais William Ruto kufikia mwafaka.

Serikali imesema vitendo kadhaa vya uharibifu wa mali na wizi vimeripotiwa. 

Soma Zaidi: Kenya inakabiliwa leo na duru mpya ya maandamano licha ya serikali kuonya kwamba haitavumilia machafuko zaidi