1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya waandishi habari 90 wahojiwa au kukamatwa Iran

9 Agosti 2023

Mamlaka nchini Iran zimewahoji au kuwakamata zaidi ya waandishi habari 90 tangu maandamano ya nchi nzima kulitikisa taifa hilo mwaka uliopita, kulingana na ripoti zilizotolewa na vyombo vya habari vya nchini humo.

Iran Teheran Protest Jina Mahsa Amini
Picha: AFP

Maandamano makubwa yalizuka mwezi Septemba 2022 kufuatia kifo korokoroni cha mwanamke  Mkurdi wa Kiiram Mahsa Amini aliekuwa na umri wa miaka 22, ambaye alikamatwa kwa madai ya kukiuka maadili ya mavazi ya wanawake nchini humo.

Mamia ya watu wakiwemo maafisa wa vikosi vya usalama waliuawa na maelfu kukamatwa kuhusiana na ushiriki wao katika kile ambacho mamlaka zimekitaja kuwa machafuko yaliochochewa na mataifa ya magahribi.

Ripoti ya gazeti la kila siku la Shargh, ikinukuu kamati ya ndani inayowasaidia waandishi habari wanaozuwiliwa, ilisema waandishi zaidi ya 90 wanashikiliwa au kuitwa kwa mahojiano katika muda wa miezi 10 iliyopita katika miji tofauti.

Wengi wao wameachiliwa kwa dhamana au kupewa msamaha, lakini hatma ya waandishi 11, wakiwemo sita wanaozuwiliwa, na watano wanaosubiri hukumu, bado haijulikani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW