1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiLibya

Zaidi ya wahamiaji 20 hawajulikani walipo Mediterrania

5 Septemba 2024

Zaidi ya wahamiaji 20 hawajulikani walipo baada ya chombo walichosafiria kuzama katika Bahari ya Mediterrania.

Uhamiaji kinyume cha sheria hulaumiwa kuchangia maafa ya wahamiaji wanaohatarisha maisha yao.
Uhamiaji kinyume cha sheria hulaumiwa kuchangia maafa ya wahamiaji wanaohatarisha maisha yao.Picha: Daniel Kubirski/picture alliance

Vyombo vya habari vya Italia vimesema watu hao walikuwa wanasafiri baharini kutoka Libya kuelekea Italia.

Taarifa zinasema walinzi wa pwani wa Italia waliwaokoa watu saba takriban kilomita 20 kusini-magharibi mwa kisiwa cha Lampedusa.

Kulingana na ripoti, boti iliyokuwa imejaa watu ilipinduka saa chache baada ya kuondoka Libya na watu walionusurika wameeleza kwamba kulikuwa na watu 28 kwenye boti hiyo na kila mmoja alilipa kati ya dola za kimarekani 500 hadi1,000 kuweza kusafirishwa na kwamba hakuna aliyekuwa na boya la kujiokoa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW