1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya wahamiaji 2,000 waingia Uingereza

2 Agosti 2026

Wahamiaji wameingia Uingereza kwa boti ndogo huku serikali ikidai kwamba idadi ya wanaovuka imepungua, lakini changamoto ya uhamiaji bado ipo.

Uhamiaji
Waziri mkuu wa Uingereza Andy Burnham amekiri kwamba bado kuna kazi zaidi katika kudhibiti uhamiaji. Picha: Jamie Wiseman/Daily Mail/dmg media Licensing/picture alliance

Zaidi ya wahamiaji 2,000 wamevuka kuingia Uingereza kwa kutumia boti ndogo tangu Andy Burnham achukue wadhifa wa Waziri Mkuu wa Uingereza, akimrithi Keir Starmer mwezi Julai.

Takwimu mpya zinaonyesha kuwa wahamiaji 326 waliwasili Jumamosi kwa boti nne, na kufikisha idadi ya waliovuka tangu wakati huo hadi 2,057.

Hata hivyo Burnham amesema mpango wa serikali wa kudhibiti uhamiaji haramu unaanza kuonyesha mafanikio, akibainisha kuwa idadi ya wanaovuka mwaka huu iko chini ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Burnham amekiri kwamba bado kuna kazi zaidi katika kudhibiti uhamiaji.  Wizara ya Mambo ya Ndani imesema operesheni za kuzuia wahalifu wanaosafirisha watu zimeongezwa, na mchakato wa kuwarudisha makwao wahamiaji wasio na vibali unaendelea.

Serikali ya Uingereza pia imetangaza ushirikiano mpya na Ufaransa wa kuimarisha doria na kukabiliana na mitandao ya wasafirishaji haramu wa watu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW