1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia bado wanatafutwa kufuatia maporomoko ya udongo Uganda

29 Novemba 2024

Zaidi ya watu 100 bado hawajulikani waliko kufuatia mkasa wa maporomoko ya ardhi yaliyotokea mashariki mwa Uganda siku ya jumatano.

Uganda |  Bulambuli-Maporomoko ya udongo
Maporomoko ya udongo huko BulambuliPicha: Nakasiita/AP Photo/picture alliance

Hadi sasa idadi za maiti ambazo zimeopolewa kutoka kwenye tope la maporomoko ya ardhi ni 18. Miili ya watu wanne ilipatikana usiku wakuamkia leo Ijumaa. Lakini kile ambacho kinaleta hofu na mashaka zaidi kadri muda unavyoyoyoma ni kwamba watu 113 hawajulikani waliko na kuna wasiwasi huenda wamefariki.

Polisi imethibitisha idadi hiyo ya watu ambao bdo wanatafutwa ili kubaini hali yao. Mwanahabari Gerald Matembo ambaye amefuatilia shughuli za uokozi akiwa eneo la tukio amezungumza na DW kwa njia ya simu.

''Unadhani ni hali gani ambapo vijiji vitano vinafunikwa na tope na watu zaidi ya mia moja hatujui kama watapatikana wakiwa hai.''

Mkasa wa kuporomoka kwa jaa la taka, Kampala

02:38

This browser does not support the video element.

Kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu wanaendelea na shughuli za kuwatafuta watu walionusurika, lakini ni watu 32 waliofanikiwa kuokolewa na kuwakimbiza kwenye vituo vya afya. Kile kinachotatiza ni hali ya hewa na barabara duni kuwezesha vifaa muhimu kufikishwa kwenye vijiji hivyo vitano. Soma pia: Kiasi ya watu 30 wahofiwa kufa kwenye maporomoko ya ardhi Uganda

Msemaji wa Shirika la Msabala Mwekundu, John Cliff Wamala amefafanua kuhusu hali ya maafa na hasara ambayo hadi sasa wamekadiria.''Makazi 45 yalifunikwa na tope na mali za watu ikiwemo mifugo na mashamba kuharibiwa. Tunaendelea na operesheni kwa usaidizi wa jeshi, polisi na wananchi.''

Soma habari inayohusiana na hiyo: Jaa la taka laporomoka Kampala na kuuwa watu 23

Watu kadhaa walionusurika wamesimulia jinsi walivyotengana na jamaa zao na wanahimiza kuwepo juhudi za kuwapata wakiwa hai au wakiwa wamefariki ili wawafanyie maziko stahiki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW