MigogoroHaiti
Zaidi ya watu 10,000 nchini Haiti wayakimbia makazi yao
25 Oktoba 2024Matangazo
Zaidi ya watu 10,000 nchini Haiti wameyakimbia makazi yao wiki iliyopita wakati magenge yenye silaha yanayofanya shughuli zao ndani na nje ya mji mkuu Port-au-Prince yakiongeza mashambulizi kwenye maeneo ambayo bado hawayadhibiti.
Takwimu hizi ni kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, jana Alhamisi.
IOM lilisema mwanzoni mwa mwezi Septemba kuwa zaidi ya watu 700,000 waliyahama makazi yao, idadi hiyo ikiwa ni karibu mara mbili ya ile ya miezi sita iliyopita.
Magenge hayo yameongeza mashambulizi wiki iliyopita, wakati sehemu kubwa ya mji mkuu na vitongoji vyake ikidhibitiwa na vikundi mbalimbali vyenye silaha vilivyoungana.