Zaidi ya 100,000 wakimbia mapigano chini ya wiki moja Kongo
8 Januari 2025Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, baina ya tarehe 1 na 3 Januari, mapigano makali kati ya jeshi na waasi wa M23 katika mji Masisi Kati, jimbo la Kivu Kaskazini, yamewahamisha makwao watu 102,000.
Wizara ya mambo ya nje ya Rwanda inadai kuwa eneo lililotwaliwa na waasi wa M23 hivi karibuni lilikuwa kwenye mikono ya wanamgambo wa Kihutu, FDLR, wanaohusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda.
Soma pia:Rais wa Kongo afanya mabadiliko makubwa jeshini
Kwenye taarifa yake, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, alilaani ukosoaji wa jamii ya kimataifa ambayo alisema imeshindwa kulaani kuendelea kukiukwa kwa mamlaka ya ardhi ya Kongo inayomilikiwa na jamii za Wakongo, wakiwemo Watutsi raia wa Kongo.