1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 100,000 wakimbia makaazi yao Kivu ya Kaskazini

Saleh Mwanamilongo
11 Januari 2025

Taarifa hiyo imetolewa na Umoja wa Mataifa ambao umetaja mapigano kati ya jeshi la Kongo FARDC na waasi wa M23 kama sababu ya hali hiyo.

Zaidi ya watu 100,000 wamekimbia makazi yao mashariki mwa Kongo tangu mwanzoni mwa mwaka huu
Zaidi ya watu 100,000 wamekimbia makazi yao mashariki mwa Kongo tangu mwanzoni mwa mwaka huuPicha: Moses Sawasawa/AP/picture alliance

Wakimbizi hao wapya wanaongeza idadi ya watu milioni 2.8 ambao tayari wameyakimbia makaazi yao katika jimbo la Kivu Kaskazini, ikiwa ni sawa na zaidi ya theluthi moja ya jumla ya wakaazi wa jimbo hilo.

Waasi wa kundi la M23 waliuteka mji wa Masisi-Centre siku ya Jumatatu, na kusababisha maelfu ya wakaazi kuuhama mji huo. M23 ni mojawapo ya zaidi ya makundi 100 yenye silaha ambayo yamekuwa yakipigana kwenye eneo la mashariki mwa Kongo.

Kwa ujumla, zaidi ya watu milioni 7 ni wakimbizi wa ndani nchini Kongo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW