Zaidi ya watu 200 wauwa kufuatia mashambulio manne ya mabomu Iraq
15 Agosti 2007Kuna wasiwasi kuwa maiti zaidi huenda zimefunikwa na vifusi vya majengo yaliyoporomoka. Mashambulizi hayo ni mabaya zaidi kuwahi kutekelezwa kwa wakati mmoja na wapiganaji katika kipindi cha miaka minne tangu kuzuka kwa vita nchini iraq.Walipuaji hao wa kujitolea mhanga waliyalipua mabomu yaliyokuwa yametegwa ndani ya malori manne katika vijiji viwili katika mkoa wa Nineveh ambayo ni makaazi ya wafuasi wa madhehebu ya kale ya Yazidi waliowachache.
Ni mashambulizi yalisababisha pia kujeruhiwa kwa zaidi ya watu 350 .Majeruhi wamelazwa katika hospitali zilizo kaskazini mwa iraq huku matabibu katika klinki za maeneo hayo wakijaribu wawezavyo kuhudumia idadi kubwa ya majeruhi.
Shughuli za ukoaji zingali zinaendelea ili kuwatafuta manusura waliofunikwa na vifusi vya nyumba zilizoporomoka kufuatia mashambulizi hayo.
Meya wa manispaa ya Sinjar Abdul Rahim al Shammari amesema zaidi ya nyumba 70 zliteketea kufutaia mashambulizi hayo na polisi wameweka sheria ya kutoka nje katika eneo la Sinjar na mji uliokaribi wa Tal Afar ambako hakukutokea mashambulizi yeyote.
Marekani imeshtumu mashambulizi hayo na kuyataja ya kinyama dhidi ya watu wasiokuwa na hatia.Hata hivyo imeapa kuyasadia majeshi ya iaraq kukabiliana na makundi kama hayo.
Waziri mkuu wa iarq Nuri ala Maliki pia ameyashtumu mashambulizi hayo na kuagiza kuanzishwa kwa uchunguzi mara moja. Wafuasi wa madhehebu ya Yazidi wanaokisiwa kuwa mamia kadha kote duniani huzumgumza na lahaja ya kikurdi lakini wanafwata dini kabla ya uislamu na wanatamaduni zao.
Wanamwamini mungu kama muumba na wanawaheshimu mitume walioko kwenye bibilia na Koran na hasa abraham lakini mtazamo wao wa kuabudu unamwalekea zaidi Malak Taus mkuu wa malaika ambaye anawakilishwa na ndege tausi.
Lakini waumini wa madhehebu mengine wanadai malaika huyo ni shetani na kusababisha dhana isiyokuwa na msingi kuwa dhehebu hilo la kisiri la yazidi wanaaabudu shetani.
Huku hayo yakijiri msichana na watu saba wenye silaha wameuawa kufuatia mapigano kati ya watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa kundi la kigaidi la al qaeda na watu kutoka kabila la wasunni katika mkoa wa Diyala kaskazini mashariki mwa Baghdad.