1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 235,000 wakimbia Idlib, Syria

27 Desemba 2019

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo imesema zaidi ya watu 235,000 wameukimbia mkoa wa Idlib katika kipindi cha wiki mbili zilizopita wakati mashambulizi ya vikosi vya serikali ya Syria na Urusi yakiongezeka.

Syrien Idlib | Syrier in Harbanos
Picha: picture-alliance/AA/M. Said

Ripoti za Umoja wa Mataifa iliyochapishwa hii leo imesema zaidi ya watu 235,000 Maelfu ya raia wakimbia mashambulizi Idlibwameukimbia mkoa wa Idlib katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, katika wakati ambapo mashambulizi ya vikosi vya serikali ya Syria na Urusi yakiongezeka katika ngome hiyo ya mwisho ya waasi nchini Syria.

Kulingana na shirika la Umoja ya Mataifa linalishughulikia masuala ya kiutu, OCHA idadi hiyo kubwa ya watu walioondoka kati ya Disemba 12 na 25 imeliacha eneo la Maaret al-Numan, kusini mwa Idlib likielekea kuwa tupu.

Mwandishi wa habari wa shirika la AFP kwenye eneo hilo ameshuhudia makundi makubwa ya watu wakikimbia katika siku za hivi karibuni. Kumeshuhudiwa malori yakisafirisha abiria katika barabara kuu inayounganisha eneo la kusini mwa Idlib na mikoa mingine iliyoko eneo la kaskazini. 

Baadhi ya watu wanaonekana wakiondoak eneo la Idlib kufuatia mashambulizi ya Syria na Urusi.Picha: Getty Images/AFP/A. Watad

Kulingana na OCHA, mashambulizi yanayoendelea yamesababisha watu hao kukimbia kutoka eneo hilo na mji wa karibu wa Saraqeb. Ripoti hiyo imesema Idlib inadhibitiwa na kundi la wanamgambo ambalo awali lilikuwa na mahusiano na kundi la al-Qaeda la Hayat Tahrir al-Sham, ambalo wiki hii kiongozi wake mkuu aliwataka wanamgambo na waasi washirika wa kundi hilo kusonga mbele katika mapambano dhidi ya kile alichokitaja uvamizi wa Urusi na serikali. 

Eneo hilo linahifadhi wakaazi wapatao milioni 3, wengi wao wakiwa ni wale waliokimbia machafuko katika maeneo mengine ya Syria. Serikali ya Damascus, ambayo kwa sasa inadhibiti asilimia 70 ya Syria mara kwa mara imeapa kulirejesha eneo hilo la Idlib.

Watu waliokimbia makaazi yao huko nchini SyriaPicha: AFP/A. Watad

Damascus inayoungwa mkono na Moscow walianzisha mashambulizi dhidi ya Idlib mwezi Aprili na kusababisha vifo vya raia 1,000 na wengine wapatao 400,000 kuyakimbia makaazi yao. Omar Hafyan ni mmoja ya wakimbizi hao, "Tulikuwa tumekaa usiku, mara tukashambuliwa na bomu. Siku iliyofuata, tuliondoka na kuacha kila kitu kwa sababu mashambulizi hayo yaliongezeka. Kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi, tulivaa nguo zetu tu na kuondoka. Tulikabiliwa na hali mbaya hadi tulipofika hapa."
 

Licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano ya mwezi Agosti vikosi tiifu kwa serikali ya Syria vimeendeleza mashambulizi dhidi ya waasi hao kusini mwa Idlib.

Rais Donald Trump wa Marekani jana aliandika kwenye ukurasa wa twitter, akiionya Syria na Urusi dhidi ya mauaji hayo ya raia wa Idlib na kusema Uturuki imekuwa ikifanya kazi kubwa kuzuia mauaji hayo.

Zaidi ya watu 370,000 wamekufa kwenye vita hivyo vya Syria na mamilioni wengine hawajulikani walipo tangu vita hivyo vilipoanza kufuatia maandamano ya kuipinga serikali ambapo waandamanaji walikabiliwa vikali na vikosi vya usalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW