1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArmenia

Waarmenia wa Nagorno Karabakh wakimbilia nchini Armenia

25 Septemba 2023

Serikali ya Armenia imesema kuwa zaidi ya watu 2,900 kutoka Jimbo la Nagorno-Karabakh wamewasili nchini humo, baada ya Azerbaijan kutangaza wiki iliyopita kuchukua udhibiti wa eneo hilo linalozozaniwa

Waarmenia wa Nagorno Karabakh wasubiri mabasi kuwasafirisha kutoka eneo hilo kuelekea nchini Armenia mnamo Septema 25, 2009
Waarmenia wa Nagorno Karabakh wasubiri mabasi kuwasafirisha kutoka eneo hiloPicha: David Ghahramanyan/REUTERS

Hapo jana, Uongozi wa Warmenia 120,000 wanaoishi Nargono Karabakh ulisema wanadhamiria kuondoka eneo hilo na kuelekea nchini Armenia, kwa kuwa hawataki kuishi katika sehemu ya Azerbaijan na pia wanahofia kuwa wahanga wa mauaji ya kikabila.

Erdogan kukutana na Aliyev

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa hii leo kukutana na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev. Viongozi hao watazungumzia miongoni mwa mambo mengine uhusiano baina ya mataifa yao lakini pia na mzozo wa sasa katika jimbo la Nagorno-Karabakh.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW