1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSenegal

Zaidi ya watu 300 wapotea baharini wakitokea Senegal

10 Julai 2023

Watu wasiopungua 300 wanaosafiri kwa kumitia boti tatu kutoka Senegal kuelekea Uhispania wamepotea baharini na hadi sasa hakuna mawasiliano yoyote yaliyofanyika na kundi hilo la watu.

Ufaransa, wahamiaji
Wahamiaji wakiwa kwenye boti pwani ya UfaransaPicha: Salmeer Al-Doumy/AFP/Getty Images

Watu wasiopungua 300 wanaosafiri kwa kumitia boti tatu kutoka Senegal kuelekea Uhispaniawamepotea baharini na hadi sasa hakuna mawasiliano yoyote yaliyofanyika na kundi hilo la watu.

Hayo yameelezwa na shirika la misaada ya kiutu la Walking Borders kupitia mratibu wa shughuli zake, Helea Maleno Garzon. Kulingana na shirika hilo, boti mbili ziling´oa nanga kutoka mji wa Mbour mnamo Juni 23 zikiwa na watu 100 na boti ya tatu iliondoa siku nne baadaye kutoka mji wa kusini mwa Senegal wa Kafountine ikiwa imewabeba takribani watu 200.

Mratibu wa shirika la Walking Borders amesema kitu muhimu hivi sasa ni kuwatafuta na kuwapata watu hao akisema wanahitaji ndege zaidi kujaribu kuwafikia. Mamlaka za Senegal na Uhispania hazijapatikana kutoa maelezo yoyote kuhusu mkasa huo.

Njia ya uhamiaji kupitia bahari ya Atlantiki ndiyo hatari zaidi duniani na takwimu zinaonesha karibu watu 800 wamekufa au kupotea baharini katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.