Zaidi ya watu 40 wafariki kwenye ajali ya barabarani Kenya
1 Julai 2023Matangazo
Picha za televisheni zimeonesha uharibifu mkubwa uliotokea kwenye eneo la mkasa huo ikiwemo mabaki ya magari madogo yaliyogongwa na lori hilo lililopinduka. Waokoaji pia walionekana wakihangaka kujaribu kuwatafuta watu wanaoaminika wamekwama kwenye mabaki ya magari yaliyopondeka. Polisi imesema ajali hiyo imetokea kwenye barabara kuu inayounganisha miji miwili ya Kericho na Nakuru.
Maafisa wa usalama wamearifu kwamba mbali ya vifo vya watu 48, wengine 30 wamejeruhiwa vibaya na waliwahishwa hospitali huku kukiwa na wasiwasi kwamba idadi inaweza kuongezeka.
Rais William Ruto wa Kenya na viongozi wengine wa taifa hilo wametuma salamu za rambirambi kufuatia mkasa huo.