1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Mafuriko yaua zaidi ya watu 500 Afrika Magharibi na Kati

16 Septemba 2024

Zaidi ya watu 500 wamefariki kufuatia mvua kubwa za mfululizo pamoja na mafuriko yaliyolikumba eneo kubwa la kanda ya Afrika ya Kati na Magharibi.

Mafuriko
Mafuriko yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 500 Afrika Magharibi na KatiPicha: El Tayeb Siddig/REUTERS

Hayo yameelezwa leo na Umoja wa Mataifa ambao umesema nchini Chad peke yake watu milioni 1 wameathirika kutokana na mafuriko hayo.

Ofisi ya uratibu wa masuala ya kiutu ya Umoja wa Mataifa-Ocha imefahamisha kwamba mafuriko yameathiri watu laki 6 zaidi nchini Nigeria na laki tatu nchini Niger.

Cameroon, Mali na sehemu za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo pia zinakabiliwa na mafuriko yaliyozifunikia barabara na mashamba pamoja na kuharibu makaazi.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW