1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 5,000 wafariki kutokana na mzingiro wa Tigray

Hawa Bihoga
27 Januari 2022

Ripoti mpya ya ofisi ya masuala ya afya katika eneo la Tigray nchini Ethiopia imesema kwamba, takriban watu 1500 walikufa kwa utapiamlo kwa mwaka jana katika eneo hilo ambalo limezingirwa na vikosi vya serikali.

IDP’s and homeless in the city of Mekele
Picha: Million Hailesilassie/DW

Ripoti hiyo inataja kwamba Vifo zaidi ya 5000 vimetokana na njaa pamoja na magonjwa hii ni kutokana na eneo hilo kuzingirwa na majeshi ya serikali. mkuu wa ofisi ya afya ya Tigray, Hagos Godefay, amenukuliwa na vyombo vya habari akisema vifo vinaongezeka kwa kiwango cha kutisha, vinavyochangiwa na magonjwa yanayoweza kuzuilika kama vile kichaa cha mbwa.

Soma pia: Shambulio la "drone" laua 17 Tigray

Tathmini ya kwanza tangu kuzuka kwa vita katika eneo hilo mnamo mwezi novemba mwaka 2020,iliyofanywa na ofisi yake pamoja na mashirika mengine ya misaada ya kibinaadamu imeonesha kuwa vifo 5,421 vilivyothibitishwa huko Tigray kati ya mwezi Julai na Oktoba mwaka 2021. vilisababishwa na utapiamlo, magonjwa ya kuambukiza na yale yasioambukiza.

Kuna changamoto kuingiza misaada TigrayPicha: DW

Kabla ya kuzuka kwa mgogoro huo eneo hilo lilirekodi watoto walio chini ya umri wa miaka 5 waliougua utapiamlo mkali ilikuwa ni chini ya asiilimia 2, katika matokeo ya tathmini hiyo mpya  kiwango kinachoshuhudiwa ni juu ya asilimia 7, huku takriban watoto 369 walio chini ya miaka 5 wamekufa kutokana na utapiamlo kati ya watu 1,479.

Hagos, amesema tathmini hiyo ya vifo ilihusisha takriban asilimia 40 ya eneo la Tigray, ambapo kutokana na baadhi ya maeneo kukaliwa na wapiganaji walishindwa kukusanya taarifa zaidi na hata kufikishwa kwa misaada ya kiutu, ikiwemo, kukosekana kwa vifaa tiba, dawa za kufubaza virusi vya ukimwi, na magonjwa yaliyoweza kuzuilika ikiwemo surua na covid-19 yalienea kwa kasi.

Mwezi Juni mwaka uliopita wakati vikosi vya wapiganaji wa Tigray viliporejesha udhibiti wa eneo hilo, serikali ya Ethiopia ilidhiditi ufikishwaji wa misaada ya kiutu ikiwemo chakula na vifaa tiba, ikihofia misaada hiyo kuangukia mikononi mwa wapiganaji, jambo ambalo limekuwa likionywa na umoja wa mataifa mara kwa mara.

Hata hivyo wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia, imesema katika taarifa yake kwamba, itafanya kazi na mashirika ya misaada ya kiutu kwa kuruhusu safari za ndege za mizigo hadi eneo hilo la mzozo la Tigray ili kusafirisha mahitaji muhimu ikiwemo dawa na vifaa tiba. hata hivyo bado ni kitendawili ni  lini safari hizo za ndege zitaanza.

afp, dpa, ap

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW