1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 50,000 wamepata chanjo ya Mpox Kongo na Rwanda

2 Novemba 2024

Zaidi ya watu 50,000 kufikia sasa wamechanjwa dhidi ya virusi vya mpox katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda, mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni amesema.

DR Kongo | mpox
Raia wa Kongo akipatiwea chanjo ya MpoxPicha: Ernest Muhero/DW

Zaidi ya watu 50,000 kufikia sasa wamechanjwa dhidi ya virusi vya mpox katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda, mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni amesema.

Mlipuko huo bado haujadhibitiwa, shirika la afya la Umoja wa Afrika limeonya na kutoa wito wa kupatikana kwa rasilimali zaidi ili kuepuka janga hilo kuwa kubwa kuliko janga la Uviko 19 la miaka michache iliyopita.

Soma zaidi. Chanjo ya mpox kuchukuwa muda mrefu zaidi Kongo

Kwa mujibu wa ripoti ya Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (CDC), zaidi ya watu 1,100 wamekufa kwa ugonjwa wa mpox barani Afrika, na takriban watu 48,000wameorodhoshwa kuwa wameambukizwa tangu Januari mwaka huu.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndio nchi iliyoathirika zaidi na ugonjwa wa mpox na inaongoza kwa idadi ya watu waliokufa na ugonjwa huo.