1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 70 wauwawa na ADF Kongo

Hawa Bihoga
15 Machi 2023

Wapiganaji wa kundi la waasi la ADF wameua zaidi ya watu 20 katika muda wa siku mbili kusini-magharibi mwa wilaya ya Beni, mashariki mwa Kongo, huku mamia ya wakaazi wakiyakimbia makazi yao.

Kongo | Demokratische Republik Kongo DRC Soldaten
Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Wapiganaji wa kundi la waasi la ADF wameua zaidi ya watu 20 katika muda wa siku mbili kusini-magharibi mwa wilaya ya Beni, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, ikiwa ni muendelezo wa mashambulizi yaliosababisha mamia ya wakaazi kuyakimbia makazi yao.

Katika vijiji vya Mabulengwe, Kininga,Vulera na Maombi wilayani Beni vilivyoshuhudia mauwaji hayo yaliyofanywa na ADF jana na juzi jumatatu.

Magaidi hao katika mashambulizi yao, waliwauwa kwa kuwakata kwa mapanga wakaazi zaidi ya ishirini, kwa mujibu wa vyanzo vya habari karibu na mashirika ya kiraia. 

Mauwaji ya jana na juzi, yamepelekea idadi ya watu waliouawa na ADF kwa kipindi cha wiki moja kufikia zaidi ya sabini. 

Mauaji yaathiri mchakato wa kidemocrasia

Mashambulizi ya kila siku katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Beni yameathiri pia zoezi la tume ya uchaguzi la kuandikisha wapiga kura katika eneo hilo.

Raia wa Kongo wakiondoka katika vijiji vyao vilivyoshambuliwa na makundi ya wapiganajiPicha: Nicholas Kajoba/Xinhua/IMAGO

kutokana na usalama mdogo zoezi hilo limesimamishwa katika kijiji cha Mabuku,

Baadhi ya wakaazi katika kijiji cha Mabuku wameiambia DW Kiswahili kwamba,raia wengi wameyakimbia maazi yao.

"Sidhani kama zoezi litaendelea watu wamekimbia, hakuna atakae weza kwenda kujiandikisha."

Alisema mkaazi huyo na kuongeza kwamba mauaji hayo yameathiri pakubwa zoezi hilo la kidemocrasia,ambapo wengi walilalamikia suala la usalama wakati zoezi hilo lilipozinduliwa.

Mapambano makali kati ya viokosi

Baada ya kuzidiwa nguvu na majeshi ya muungano yaani UPDF na FARDC katika eneo la mashariki ya Beni, baadhi ya wapiganaji wa ADF walikimbia uwanja wa mapambano.

Wapiganaji hao walielekea katika eneo la kusini magharibi mwa Beni, ambako inaonekana kwamba hakuna wanajeshi wa kutosha. 

Mashirika ya kiraia katika eneo hilo, yameiomba serikali kuwatuma haraka wanajeshi wa FARDC pamoja na UPDF.

Mashirika hayo yameripoti katika eneo la kusini magharibi, wapiganaji wa ADF wanaowauwa watu pamoja na kuteketeza mali. 

Serikali ya Kongo tayari imeonesha utayari wa kutuma vikosi katika maeneo hayo ambayo hali ya usalama inazidi kutetereka.

kupitia waziri wa elimu ya juu pamoja na vyuo vikuu Nzangi Butondo,alisema katika masaa machache, majeshi ya muungano yatatumwa katika maeneo yanayowahifadhi ADF yaani kusini mwa Beni. 

Waasi M23 waondoka Kabumba

02:42

This browser does not support the video element.

"Wanajeshi wa muungano watapelekwa haraka katika maeneo yanayolengwa na mashambulizi ya ADF"

 Butondo alisema katika kipindi cha mdahalo cha radio Okapi,na kuongeza kwamba ADF wamehatarisha usalama katika eneo hilo pamoja na uüpande wa mbuga ya Virunga.

Wachambuzi: ADF wanazidi kuhatarisha usalama Beni 

Hali ya usalama kwenye barabara ya Beni kwenda Butembo kusini mwa mji huo bado ni tete.

Wachambuzi wa masuala ya usalama wanasema, kukimbia kwa wakaazi wa vijiji vilivyoko kwenye barabara hiyo, huenda kukawapa nafasi ADF, kujijenga zaidi na kuendeleza ukatili wao dhidi ya raia wasiokuwa na hatia. 

Tangu mwaka we elfu mbili na kumi na nne, ADF wameshawauwa maelfu ya watu katika wilaya za Beni, Irumu pamoja na Mambasa, na haijulikani mauwaji hayo yatakomeshwa lini. 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW