1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 80 wamekufa kutokana na ajali ya boti Kongo

13 Juni 2024

Watu 86 wamekufa katika ajali ya boti iliyotokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Hayo yametangazwa na ikulu ya nchi hiyo jioni ya jana Jumatano.

Watu zaidi ya 80 wamekufa kutokana na ajali ya boti Kongo
Watu zaidi ya 80 wamekufa kutokana na ajali ya boti KongoPicha: Junior Kannah/AFP/Getty Images

Haijabainika wazi boti hiyo ilikuwa imewabeba abiria wangapi. Kamishna wa mamlaka wa mto huo Ren Maker amesema ajali hiyo ilitokea gizani, akiongeza kuwa pengine boti hiyo ilipata hitilafu ya injini na ilizama baada ya kugongwa na boti nyingine.

Maker amesema, watu kadhaa waliruka majini wakati boti ilipoanza kuzama na wakamudu kujiokoa. Rais Felix Tshisekedi amesema amefadhaishwa na mkasa huo na kuamuru uchunguzi ufanyike kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Ajali za boti hutokea mara kwa mara nchini Kongo kutokana na nyingi kupakia kupindukia uwezo, matengenezo duni na sheria dhaifu za kusimamia uendeshaji wa vyombo vya majini.