Zaidi ya watu bilioni 1 duniani ni wanene kupindukia
1 Machi 2024Jarida hilo linasema idadi hiyo imeongezeka zaidi ya mara nne tangu mwaka 1990.
Utafiti huo uliofanywa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) unaonesha kwamba "janga" hilo hasa linazikumba nchi maskini duniani na idadi inaongezeka kwa haraka zaidi miongoni mwa watoto na mabaleghe kuliko kwa watu wazima.
Soma zaidi: Ripoti: Dunia itakuwa na watu wanene kupita kiasi 2035
Utafiti huo uliotolewa kuelekea maadhimisho ya Siku ya Unene wa Kupitiliza mnamo Machi 4, unakadiria kwamba kulikuwa na karibu watu wazima, mabaleghe na watoto milioni 226 waliokuwa na unene wa kupita kiasi mwaka 1990.
Kufikia mwaka 2022, idadi hiyo ilikuwa imeongezeka na kufikia watu bilioni moja milioni 38.
Mkurugenzi wa lishe kwa ajili ya afya katika shirika la WHO, Francesco Branca, amesema ongezeko hilo la kuvuuka bilioni moja limetokea mapema zaidi kuliko makadirio waliyokuwa nayo.