1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu milioni nne wameyakimbia makazi yao Ethiopia

24 Agosti 2023

Takwimu mpya za Umoja wa Mataifa zimeonesha zaidi ya watu milioni nne wameyakimbia makaazi yao nchini Ethiopia kutokana na mzozo na ukame.

Sudan EU richtet humanitäre Luftbrücke in den Sudan ein
Picha: Amanuel Sileshi/AFP

Ripoti ya Shirika la Wahamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM, kuhusiana na watu wanaoyakimbia makaazi yao nchini humo imesema jumla ya watu milioni 4.38 wameyakimbia makaazi yao kuanzia Disemba 2022 hadi Juni 2023.

Kulingana na ripoti hiyo iliyochapishwa jana Jumatano, mizozo iliongoza kwa kuchochea tatizo hilo kwa asilimia 66.41 na ukame ukichangia kwa asilimia 18.49.

Zaidi ya watu milioni moja waliukimbia mkoa wa Tigray uliokumbwa na machafuko.

Jumla ya watu milioni 28 nchini Ethiopia wanahitaji msaada, hii ikiwa ni kulingana na takwimu za umoja huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW