1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Zaidi ya watu nusu milioni wamekimbia makazi yao Lebanon

5 Oktoba 2024

Shirika la OCHA limesema idadi ya vifo vinavyotokana na mgogoro imeripotiwa kuongezeka kwa asilimia 200 katika wiki mbili zilizopita, huku watu waliokimbia makazi wakiongezeka kwa asilimia 385.

Watu 285,000 wameondoka nchini Lebanon kufuatia mashambulizi ya Israel
Watu 285,000 wameondoka nchini Lebanon kufuatia mashambulizi ya IsraelPicha: Houssam Shbaro/Anadolu/picture alliance

Kulingana na shirika la OCHA,likitaja wizara ya afya ya Lebabon ni kwamba, kufikia Alhamisi, takriban watu 1,699 wameripotiwa kuuawa na karibu elfu kumi walijeruhiwa katika vita kati ya Israel na Hezbollah ndani ya mwaka mmoja.

Wakati huohuo, jeshi la Israel limesema kuwa limewaua wanamgambo wawili kutoka kundi la Hamas katika mashambulizi huko Lebanon. Huku likiendelea na mashambulizi yake ya anga kusini mwa mji wa Beirut pamoja na Syria.

Kwa upande wake, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amehimiza kusitishwa kwa usafirishaji wa silaha kwa Israel. Macron amesema kipaumbele ni suluhisho la kisiasa.