1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zambia kuwa mwenyeji wa mkutano wa kikanda kuhusu DRC

3 Januari 2026

Zambia inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa ukanda wa Maziwa Makuu wiki ijayo, ili kujadili hali ya usalama inayozidi kuyumba katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

RWANDA-BUGARAMA-DRC-Wakimbizi
Wakimbizi wa Kongo katika mji wa BugaramaPicha: picture alliance / Xinhua News Agency

Zambia inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa ukanda wa Maziwa Makuu wiki ijayo, ili kujadili hali ya usalama inayozidi kuyumba katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yenye migogoro.

Katika taarifa yake iliyoitoa siku ya Jumamosi, Lusaka imesema mkutano huo utafanyika kwa siku tatu kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama eneo la mashariki mwa DRC, kufuatia ombi la Jumuiya ya Kimataifa ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR).

Nchi za ukanda huo zimeingiwa na wasiwasi kutokana na ghasia zinazoendelea, ambazo mwishoni mwa juma hili, zimehusisha mapigano kati ya wapiganaji wa kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda na vikosi vya DRC karibu na mji muhimu na wenye rasilimali nyingi wa Uvira, unaopakana na Rwanda.

Eneo hilo limekuwa likikumbwa na migogoro ya mara kwa mara kwa zaidi ya miongo mitatu, na ghasia zimeongezeka tangu kuibuka tena kwa M23 mwaka 2021. Zambia inapakana kwa sehemu kubwa na DRC.