1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zambia na Kongo zafungua tena mpaka wao

13 Agosti 2024

Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zimekubaliana kufungua tena mpaka wao Jumatatu, baada ya kutatua mzozo wa kibiashara uliopelekea Zambia kuufunga upande wake mwishoni mwa wiki.

Kongo| Mpaka wa Kasumbalesa
Mpaka wa Kasumbalesa kati ya DR Kongo na ZambiaPicha: Marc JourdierAFP

Waziri wa biashara na viwanda wa Zambia Chipoka Mulenga alikutana na maafisa wa serikali ya Kongo katika mji wa Lubumbashi karibu na mpaka huo.

Zambia ilitangaza Jumapili kuwa ilikuwa imefunga mpaka na Kongo, baada ya Kongo kupiga marufu ya uingizaji wa vinyaji baridi kutoka Zambia.

Soma pia: Kongo yaanzisha mazungumzo na Zambia kufungua mpaka

Hatua hiyo ilisababisha maandamano ya madereva wa malori wa Kongo karibu na mji wa mpakani wa Kasumbalesa, huku makundi nchini Zambia pia yakikosoa marufuku ya Kongo.

Chama cha wenye viwanda nchi humo kilisema marufuku hiyo inaweza kuweka mfano hatari kwa uhusiano wa baadae wa kibiashara.

Uamuzi wa Zambia kufunga mpaka wake ulitishia kuathiri uwezo wa Kongo kusafirisha nje madini yake ya dhahabu, shaba na cobalt yanayopitia Zambia kwa sehemu kubwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW