1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zambia yahalalisha usafirishaji wa bangi kukuza uchumi

Sylvia Mwehozi
17 Desemba 2019

Zambia imehalalisha uzalishaji na usafirishaji wa bangi kwa matumizi ya kiafya na kiuchumi. Kiongozi wa Chama cha upinzani Peter Sinkamba, amesema hatua hiyo inaweza kuipa Zambia Dola bilioni 36 kwa mwaka.

Kanada Legalisierung von Cannabis | Cannabis Pflanzen
Picha: picture-alliance/empics/The Canadian Press/R. Ward

Zambia imehalalisha uzalishaji na usafirishaji wa bangi kwa matumizi ya kiafya na kiuchumi. Tangazo hilo limetolewa siku ya Jumatatu na msemaji mkuu wa serikali ya nchi hiyo Dora Siliya baada ya makubaliano ya mkutano maalumu wa baraza la mawaziri.

Zambia inakuwa moja kati ya nchi ambazo hivi karibuni zimebadili msimamo wake juu ya bangi, ili kukuza uchumi wake. Nchi hiyo imehamasika kufanya hivyo kutokana na upungufu wa fedha na deni linaloendelea kukua.

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2018 deni la nje la Zambia lilikuwa limefikia dola za kimarekani bilioni 10.5  kutoka bilioni 8.74.

Kiongozi wa Chama cha upinzani cha kijani Peter Sinkamba, ambaye amekuwa akihamasisha uuzwaji wa bangi tangu mwaka 2013, amesema hatua hiyo inaweza kuiingizia Zambia kiasi cha Dola bilioni 36 kwa mwaka.