JamiiZambia
Zambia yahitaji msaada kukabiliana na ukame
17 Aprili 2024Matangazo
Wito huo umetolewa na Rais Hakainde Hichilema katika hotuba yake kwenye televisheni, akisema takriban nusu ya watu milioni 20 wa taifa hilo la kusini mwa Afrika wameathiriwa vibaya na kiangazi cha muda mrefu kilichosababishwa na tukio la hali ya hewa la El Nino.
Zambia imepata mvua ndogo mwaka huu, na hivyo kuzidisha hali ya ukame mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa. Rais Hichilema amesema ukosefu wa mvua umeharibu sekta ya kilimo na kuathiri mazao.
Rais huyo ameendelea kusema kuwa zaidi ya watu milioni 6 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu, lakini Zambia ambayo ilitangaza ukame kuwa janga la kitaifa mwezi Februari, ina takriban dola milioni 51 tu kati ya dola milioni 940 zinazohitajika ili kukabiliana na mgogoro huo.