Zambia yawafukuza Wachina 30 kwa wizi wa madini
7 Juni 2017China ilikuwa imeilalamikia Zambia, ikisema hakuna ushahidi wa kutosha dhidi ya Wachina hao 31, miongoni mwao akiwemo mwanamke mwenye mimba na mgonjwa wa Malaria.
Hata hivyo, idara ya uhamiaji ya Zambia ilikuwa imesisitiza kuwa Wachina hao watafukuzwa nchini Zambia.
China imewekeza kiasi cha dola bilioni moja katika sekta ya madini nchini Zambia, lakini Wachina wanachukiwa na Wazambia kwa tuuma za kuwanyanyasa na kuwalipa mishahara duni.
Mwaka 2012, wafanyakazi walimuuwa msimamizi wao mmoja wa Kichina na kumjeruhi vibaya mwingine katika mzozo wa malipo kwenye mgodi wa makaa ya mawe.
Mwaka mmoja kabla, polisi ya Zambia ilikuwa imewatuhumu wasimamizi wa Kichina kwa jaribio la kuuwa, baada ya Wachina hao kufyatua risasi katika mzozo mwingine wa malipo.