1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar. Chama cha upinzani chalaumu tume kwa kutotoa maamuzi.

14 Septemba 2005

Wakati kampeni za uchaguzi mkuu nchini Tanzania utakaofanyika Oktoba mwaka huu zikiendelea, chama cha upinzani cha Jahazi Asilia huko Zanzibar , kimelalamika juu ya kile ilichosema kuwa ni mazingira yasiyo mazuri ya uchaguzi, hali inayosababishwa na chama tawala CCM pamoja na tume , ambapo kimedai maamuzi yake yana ushawishi mkubwa wa serikali ya visiwani humo.

Akizungumza na radio Deutsche Welle leo, mgombea wa kiti cha urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho, Bwana Mussa Haji Kitole aliitaka serikali itowe uamuzi na kuitaka tume ihakiki daftari la kudumu la wapiga kura , ili kuondoa malalamiko yaliyopo juu ya kuongezwa kwa idadi ya watu kinyume na ile ya awali, ikiwa ni baada ya serikali kuvunja mkataba na kampuni ya Afrika kusini iliyopewa jukumu la kusimamia orodha ya walioandikishwa.

Bwana Kitole hali kadhalika amesema vitendo vya kupigwa wapinzani na wanamgambo wanaojulikana kama Janjaweed vinatishia hali ya usalama visiwani humo.

Amesema wakati serikali inasema kuwa matukio hayo yanafanywa na wahuni na kwamba wanamgambo hao si kikosi cha serikali , inashindwa kuwadhibiti wala kuwapa ruhusa wapinzani kuwadhibiti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW