Zanzibar: Hali ya viongozi wa Uamsho gerezani
8 Novemba 2012Matangazo
Mawakili wa Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI ) wamesema hii leo kuwa wateja wao waliokamatwa siku 17 zilizopita kwa tuhuma za kuchochea vurugu kisiwani Unguja, hawatendewi haki na wanapata mateso makubwa gerezani wanakoshikiliwa.
Mawakili hao wakiongozwa na Salim Tawfiq wanasema kwa sasa wateja wao hawapaswi kutendewa visa kama hivyo kwa kuwa bado ni watuhumiwa na kwamba hawajatiwa hatiani.
Muda mfupi uliopita Amina Abubakar amezungumza na wakili Salim Tawfiq na kwanza anaelezea zaidi juu ya mateso hayo wanayopata wateja wake.
(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi Amina Abubakar
Mhariri Yusuf Saumu