1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZANZIBAR : Hamad ashutumu uchaguzi kuwa sio huru na wa haki

1 Novemba 2005

Kiongozi wa upinzani Zanzibar ameshutumu matokeo ya uchaguzi wa mwishoni mwa juma wa rais na baraza la wawakilishi kuwa haukuwa huru na wa haki.

Akizungumza na waandishi wa habari hapo jana ametaka tume ya uchaguzi Zanzibar isite kutowa matokeo ya uchaguzi huo hadi pale kasoro hizo zilizojitokeza zimepatiwa ufumbuzi.Amesema takriban watu 80,000 wamenyimwa haki yao ya kupiga kura na kwamba katika majimbo kadhaa vikosi vya serikali ya mapinduzi Zanzibar vilipeleka mamia ya watu kupiga kura ambapo wakaazi wa maeneo husika wamesema hakuwastahiki kupiga kura.

Amesema matokeo hayo yamepikwa na kulaumu kutiwa mkono kwa orodha ya wapiga kura na kutokuwepo kwa makaratasi ya matokeo.

Hamad amesema iwapo itathibitika kwamba kumekuwepo mizengwe kwenye uchaguzi huo ataitisha maandamano makubwa ya amani mithili ya yale ya Ukaraine kudai ushindi wao ulioporwa.

Maelfu kwa maelfu ya wafuasi wa chama chake cha CUF walikusanyika kwenye makao makuu ya chama hicho kusubiri maelekezo kutoka kwa viongozi wao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW