1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar. Kagame awataka wazanzibari kudumisha amani kabla ya uchaguzi wa Oktoba.

14 Mei 2005

Rais wa Rwanda Bwana Paul Kagame jana alitoa wito wa amani katika eneo lenye hali tete ya kisiasa nchini Tanzania katika kisiwa cha Zanzibar, ambacho kimekumbwa na ghasia za kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Katika mkutano wa faragha na rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, Bwana Kagame amewataka wananchi wa Zanzibar kujitahidi kuliweka eneo la Afrika mashariki kuwa la amani, kabla ya uchaguzi mkuu hapo Oktoba 30.

Chama tawala cha CCM na kile cha upinzani Civic United Front CUF, vilitia saini makubaliano ya muafaka mwaka 2001 baada ya karibu watu 40 kuuwawa katika mapambano kati ya polisi na waandamanaji wa chama hicho cha upinzani wakati wa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2000.

Lakini kabla ya uchaguzi wa hapo Oktoba 30, ghasia kati ya wanachama wa vyama hivyo viwili hasimu zimeanza tena, na kila mara zikichafua mwenendo wa uandikishwaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali katika kisiwa hicho.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW