1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZANZIBAR: Ndizi zapigwa marufuku

24 Agosti 2006

Maofisa kisiwani Zanzibar wamepiga marufuku ununuzi wa ndizi kutoka nje kuzuia kuzuka kwa ugonjwa hatari unaoharibu na kuua migomba.

Kamishna wa kilimo kisiwani humo, Mberek Rashid Saidi, amesema sasa ni kinyume cha sheria kuagiza aina yoyote ya ndizi mbichi au mbivu, majani na mbegu kisiwani humo.

Saidi amesema atakayevunja sheria hiyo atatozwa faini ya shilingi elfu 50 pesa za Tanzania au afungwe gerezani kwa miezi mitatu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW