1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZANZIBAR: Rais aapishwa

2 Novemba 2005

Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar ameapishwa leo baada fujo na vurugu kukumba uchaguzi kisiwani humo.

Chama kikuu cha upinzani cha CUF kimesema wafuasi wake kadhaa wameuwawa kufuatia makabiliano na polisi katika kisiwa cha Pemba.

Serikali pia imetoa taarifa kuwa maafisa wanne wa usalama wameuwawa katika vurugu hizo.

Chama cha upinzani kimesema kwa mara nyingine chama hicho kimepoteza nafasi ya kuing’oa serikali ya CCM kutokana na wizi wa kura.

Wakaguzi wa kimataifa wameeleza kutoridhishwa na ghasia zilizotokea wakati wa uchaguzi lakini wanaafikiana na matokeo ya uchaguzi huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW