1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar. Uchaguzi mkuu waahirishwa.

28 Oktoba 2005

Tanzania imeahirisha jana uchaguzi mkuu wa taifa uliopangwa kufanyika mwishoni mwa juma hili , baada ya kifo cha mgombea wa upande wa upinzani.

Jumbe Rajab Jumbe , mwenye umri wa miaka 65 mgombea mwenza wa chama cha tatu kwa ukubwa , nchini Tanzania cha Chadema, amefariki siku ya Jumatano usiku kwa ugonjwa wa mshtuko wa moyo, na kusababisha maafisa wa tume ya uchaguzi kufanya mkutano mkutano mrefu wa dharura ili kuweza kutafakari nini cha kufanya.

Uchaguzi huo kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Louis Makame utafanyika hapo Desemba 18.

Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa uahirishaji huo unatarajiwa kuwa utachelewesha tu ushindi mkubwa wa chama tawala, katika upande wa bara , chama ambacho kimetawala taifa hilo la Afrika mashariki kwa muda wa miongo minne.

Lakini uchaguzi huo utavuta hisia za kimataifa zaidi katika kisiwa cha Zanzibar , ambako chama tawala cha CCM kinakabiliana na mpambano mkali dhidi ya chama cha upinzani cha CUF.

Msemaji wa tume ya uchaguzi katika kisiwa cha Zanzibar Idrissa Jecha amesema uchaguzi katika kisiwa hicho utafanyika siku ya Jumapili kama ulivyopangwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW