1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZANZIBAR: Wakazi wa Zanzibar wapiga kura hii leo

30 Oktoba 2005

Wapiga kura visiwani Zanzibar nchini Tanzania hii leo wanapiga kura kumchagua rais pamoja na baraza la wawakilishi na madiwani wao.Vituo vya kupigia kura vinatazamiwa kufunguliwa saa moja asubuhi na kubakia wazi hadi saa kumi na moja jioni.Matokeo hayatazamiwi kupatikana kabla ya kati kati ya wiki ijayo.Uchaguzi unafanywa Zanzibar kama ilivyopangwa,licha ya kuwa Tanzania Bara,uchaguzi huo umeahirishwa hadi Desemba 18 kwa sababu ya kifo cha mgombea mwenza wa urais wa chama cha upinzani-Chadema,bwana Jumbe Rajab Jumbe.Siku ya jumamosi wanasiasa wa chama tawala cha CCM na wa chama cha upinzani CUF,walikuwa na mikutano ya hadhara wakifanya kampeni za mwisho kuvutia wapiga kura.Kiasi ya polisi na wanajeshi 35,000 wametawanywa Zanzibar na vile vile idara ya kutoa huduma za dharura imejiandaa pindi kutazuka mapambano kama ilivyokuwa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2000.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW